HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SERIKALI YAAGIZA TAMRISO KUGAWA MIRABAHA 2025


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeielekeza 

Kampuni ya Kukusanya na Kugawa Mirabaha ya Tanzania Music Rights Society (TAMRISO),  kuhakikisha wanafanya mgao wa mirabaha unaotarajiwa kufanyika mwanzoni mwa mwaka 2025 kwa makusanyo ya 2023/2024 na 2024/2025 (Julai hadi Disemba).

Maagizo hayo yametolewa na Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘MwanaFA’, Jijini Dar es Salaam.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Kampuni hiyo iliyoundwa na Wasanii wa Muziki, ndiyo yenye jukumu la kukusanya na kugawa mirabaha hiyo ya Wasanii.


#KAZIINAONGEA

Post a Comment

0 Comments