HEADLINES

6/recent/ticker-posts

HALOPESA YAADHIMISHA MIAKA TISA KWA KUTOA MAHITAJI HAYA MWANANYAMALA


 Na Amedeus Somi,
DAR ES SALAAM.

Katika kuathimisha miaka 9 tangu kuanzishwa kwa huduma za  Halopesa nchini Tanzania Taasisi hiyo imetoa msaada wa vitimwendo (Wheel Chair) 15 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa ya Mwananyamala iliyopo Jijini Dar es Salaam.

Akitoa neno la shukrani Katibu wa Afya wa Hospitali hiyo Lilian Mwanga amesema kwa jambo walilofanya Halopesa  ni lenye umuhimu mkubwa sana hospitalini hapo kwani dhana hizo zitawasaidia sana katika huduma akiwaomba wengine kujitokeza kwa ajili ya msaada zaidi hospitalini hapo kwani bado mahitaji ni mengi.
"Kwa niaba ya uongozi wa Hospitali ya Mkoa ya Mwananyamala tunashukuru sana Halopesa kwa kuwa mmeona umuhimu wa kurudisha kwa jamii na hizi Wheel Chair ni ifaa muhimu sana kwa wagonjwa hasa kumtoa sehemu moja na kumpeleka sehemu nyingine, Hospitali ya Mwananyamala ni hospitali ambayo inatumiwa na watanzania wa kipato cha chini na wa kiwango cha kati na wengi wao wamekuwa wakihitaji huduma za matibabu kwa kuchangia kidogo au wengine kwa kuhitaji huduma za bure kabisa".

Akizungumza wakati wa kukabidhi viti hivyo Mkurugenzi Mkuu wa Halopesa Nghiem Thong amesema Mfanikio ya miaka 9 sio ya kibiashara pekee bali pia ni nafasi ya kutambua wajibu wao kwa jamii na msaada huo ni dhamira ya Halopesa ya kuunga mkono sekta ya afya na kuboresha mazingira ya wagonjwa wenye uhitaji maalum pamoja na kusaidia jamii katika nyanja mbalimbali.

Nae Naibu Mkurugenzi wa Halopesa Magesa Wandwi amesema miaka tisa ya Halopesa ni ushahidi wa uhusiano wao karibu na jamii.

"Tunaamini mafanikio halisi hupatikana pale tunapochangia kutatua changamoto zinazowakabili wananchi, msaada huu sio wa kifedha tu bali ni ujumbe wa mshikamano na dhamira ya kweli na kujenga jamii bora". 

Afisa Masoko wa Halopesa Aidati Lwiza amesema Halopesa itaendelea kushirikiana na jamii katika nyanja za kimawasiliano na huduma za kifeda zilzoboreshwa ambazo zitawakwamua katika masuala ya kiuchumi.




Post a Comment

0 Comments