HEADLINES

6/recent/ticker-posts

SOMO LA ELIMU YA BIASHARA KUSAIDIA KUJENGA UJUZI KWA WAHITIMU NCHINI


 Na Mwandishi Wetu,
DAR ES SALAAM.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dkt. Aneth Komba amesema somo la Elimu ya Biashara ni la lazima kulingana na maboresho ya Mtaala ulioanza kutekelezwa Januari mwaka jana.

Akifungua kikao kazi cha siku mbili cha Makatibu Tawala wa Mikoa na maafisa Elimu kilicholenga kujadili maboresho katika Sekta ya Elimu jijini Dar es Salaam, Dkt. Komba amesema, Serikali kupitia Wizara ya Elimu Sayansi na Teknolojia imeanza kutekeleza sera iliyoboreshwa ya mwaka 2014, toleo la 2023 pamoja na mtaala iliyoboreshwa ya mwaka 2023.

Amesema maboresho ya Mitaala yako ya aina  mbalimbali ikiwemo kuanzishwa kwa somo jipya la lazima kwa wanafunzi wote wa kidato cha kwanza katika mkondo wa amali na wa jumla la Elimu ya Biashara na Elimu ya lazima ya miaka 10.
"Maboresho yanayoendelea yataleta faida mbalimbali ikiwemo kumuwezesha mhitimu kutumia maarifa ya masuala mtambuka, kuyamudu maisha na mazingira yanayomzunguka, kutumia ujuzi na stadi kumwezesha kujiajiri kuajiriwa na kuyamudu maisha na mazingira yanayomzunguka, kuendeleza fikra za ujasiliamali kwa wanafunzi kukuza maadili katika shuguli za kiuchumi, kuwajengea wanafunzi uelewa kutekeleza na kuthamini shughuli za biashara.
"Malengo ya maboresho yanaiandaa jamii kuwa na vijana wanaoweza kujiamini, kuajirika, kuajiri wengine na kuchangia kikamilifu katika maendeleo ya kiuchumi na taifa," amesema.

Naye, Afisa Elimu wa Mkoa wa Dar es Salaam Bi. Eva Mosha amekiri umuhimu wa mabadiliko kwa somo la biashara kuwa la lazima nchini kwani litasaidia kumuandaa mtoto kuwa na fikra za kujiajiri mapema.

Amesema, katika kufanikisha maboresho kwenye Sekta ya Elimu, Serikali imeajiri walimu wapya wa somo la biashara ili kuhakikisha utekelezaji wa eneo hilo, huku ikishirikiana na Shirika lisilo la Kiserikali la Educate.


Post a Comment

0 Comments