HEADLINES

6/recent/ticker-posts

PROFESA NOOR ASISITIZA MATUMIZI YA KISWAHILI AIPONGEZA TET


 Na Mwandishi Wetu,

MHADHIRI, Mwandishi wa vitabu na Mchoraji Maarufu  wa Chuo Kikuu cha Sultan Quaboos  cha nchini Oman, Profesa Ibrahim Noor ameishukuru serikali kuendeleza jitihada za  kuitangaza Lugha ya Kiswahili duniani kote na kuwaomba watanzania wote nchini kukuza lugha ya Kiswahili ili izungumzwe na watu wengi duniani kote.

Ameyasema hayo leo Aprili 12, 2025 wakati akiwasili nchini kutokea Mascut kupitia Zanzibar amesema kiswahili ni lugha yenye kupendwa na kuzungumzwa na wengi duniani kote na kuwaomba watanzania wote duniani kuendelea kutangaza kiswahili.

“Lugha hii imekuwa kubwa na kupendwa na watu wengi nchini, hivyo nawaomba wote duniani tuendelee kuunga mkono juhudi za watu waliotangulia kukitangaza Kiswahili  na wengine waendelee zaidi” amesema Profesa Noor. 

Kwa mujibu wa Profesa Noor, kuanzishwa kwa Tuzo za Uandishi Bunifu wa Mwalimu Nyere ni kuthamini  jitihada za kukuza kiswahili na kuchochea usomaji nchini.

Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk. Aneth Komba aliongoza mapokezi ya Profesa Noor akiwa sambamba na Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo za Uandishi Bunifu wa Mwalimu Nyerere, Profesa Penina Mlama na watumishi wengine wa  TET. 

Profesa Noor ni mgeni maalumu atakayeshiriki hafla ya Tuzo ya Taifa ya Mwalimu Nyerere ya Uandishi Bunifu itakayofanyika kesho Aprili 13, 2025 ambapo mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Dk. Philip Mpango.

Tuzo hizo zitafanyika kwa mara ya tatu mfululizo, mwaka huu washindi watapatikana kwenye nyanja tatu ambazo ni Ushauri, Tamthilia, hadithi za watoto na Riwaya huku washindi wakikabidhiwa zawadi za pesa taslimu na vyeti.

Post a Comment

0 Comments