HEADLINES

6/recent/ticker-posts

TWCC YATOA SIRI YA KUUZA SABASABA KWA WAFANYABIASHARA WANAWAKE


 Na AMEDEUS SOMI,
DAR ES SALAAM.

Chemba ya wafanyabiashara wanawake Tanzania  TWCC Imeendesha semina ya mafunzo kwa wafanyabiashara wanawake ili kuwapa mbinu za kufanya biashara kiushindani ili kupata faida katika maonesho ya 49 ya kimataifa ya biashara yanayotarajia kuanza Juni 28 hadi Julai 13 mwaka huu Jjijini Dar es Salaam.

Akizungumza Jijini Dar es Salama wakati wa kufunga semina hiyo Mkurugenzi wa Chemba ya wafanyabiashara wanawake nchini TWCC Dkt. Mwajuma Hamza amesema zipo mbinu nyingi wanawake wanaweza kuyazingatia ili kufanikiwa katika maonesho hayo ikiwemo nidhamu ya biashara.

Aidha Hamza amesema mfanyabiashara anatakiwa kutumia fursa ya kuwepo katika banda la TWCC kumsaidia kukua kibiashara.

Mwajuma ameeleza mambo ambayo watayaendesha wakiwa katika maonesho hayo kama vile kusaidia wanawake kufanya usajili wa biashara nk.

Mafunzo hayo ya utoaji elimu kwa wafanyabiashara watakaoshiriki maonesho ya Kimataifa ya Biashara ya Dar es Salaam International Trade Fair maarufu kama sabasaba yamepambwa na kaulimbiu ya Jiandae kwa mafanikio ya maonesho ya biashara, Uwe Tayari, Kuwajibika, uza zaidi.




Post a Comment

0 Comments