Na Amedeus Somi,
Maelezo.
Mhadhiri katika Shule ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dkt. Egbert Mkoko, amesema vyombo vya habari vitakakiwa kuepuka maudhui ya chuki, ubaguzi, kashfa, matusi na kuchochea vurugu katika kuripoti Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.
Ameyasema hayo leo Agosti 21, 2025 Jijini Dar es Salaam, wakati akitoa mada ya mwongozo wa Waandishi wa Habari katika uandishi wa habari za uchaguzi kwenye mkutano wa Wadau wa Sekta ya Habari na Utangazaji Kanda ya Mashariki kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025.
"Waandishi wa habari wanao wajibu wa kuchapisha habari za kweli, sahihi na zinazoweza kuthibitishwa, na kuongeza kuwa wanatakiwa kuepuka kujihusisha au kuwa sehemu ya wanachama wa vyama vya siasa kwa kuvaa sare za vyama, kuepuka kupokea rushwa,zawadi au takrima pamoja na kuepuka kuingia katika vituo vya kupigia kura bila kibali na kuepuka kutangaza matokeo ya uchaguzi kabla ya tume huru kutangaza".
Mwongozo huo ulioandaliwa na Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mamlaka ya MawasilianoTanzania (TRCA), Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari (JAB) na Idara ya Habari-MAELEZO kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Shule Kuu ya Uandishi wa Babari na Mawasiliano kwa Umma kupitia Shule Kuu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma (SJMC), umewataka waandishi kuepuka kubashiri matokeo, kupendelea na kueneza uvumi na madai yasiyothibitika.
0 Comments